Pages

Ads 468x60px

Featured Posts

Monday, September 1, 2014

PICHA 30 ZA KILI TOUR TANGA NI NOMAAAA....




Tamasha la Kili Music Tour limekamilisha awamu ya kuzunguka mikoani kwa show iliyofana katika uwanja wa Mkwakwani Tanga. Tamasha hilo linalidhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager lilipambwa na burudani toka kwa wasanii wanaofanya vizuri nchini wakiongozwa na malkia wa mipasho Khadija Kopa na mfalme wa taarab Mzee Yusuph ambao waliongoza kundi la wasanii kumi kutoa burudani kwa wakazi wa Tanga.

Tamasha hili sasa linarejea jijini Dar es Salaam ambapo Jumamosi Septemba 6 litahitimishwa katika viwanja vya Leaders Club.
 Umati wa mashabiki ukisubiria kwa hamu burudani uwanja wa Mkwakwani.

 Backstage: Nikki wa Pili na Ommy Dimpoz

 Backstage: Profesa Jay

Ommy Dimpoz ndiye aliifungua pazia la burudani Mkwakwani.

  Richard Mavoko akiimba kwa hisia katika Kili Music Tour Tanga

Saturday, August 23, 2014

WASANII WATAKAOTUMBUIZA TAMASHA LA FIESTA 2014 JIONI YA LEO JIJINI TANGA WAMJULIA HALI MZEE NJENJE NYUMBANI KWAKE SAHARE

 Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,almaarufu kama Mzee Njenje akizungumza machache mbele ya wasanii mbalimbali wa bongofleva waliofika nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga,kumjulia hali kutokana na maradhi yake yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa. 
Mzee Njenje amewaasa wasanii hao ambao amekiri wazi kuwa wanafanya vizuri katika anga ya muziki wao,kupata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo na suala la kutoendekeza masualaua ya anasa kama vile ulevi,ngono na mengineyo ambayo huchangia kuporomoka kwa wasanii wengi,amesema kuwa Muziki wa sasa una ushindani mkubwa hivyo kila msanii anapaswa kujituma kwa namna anayoona inafaa ili kutimiza malengo yake sambamba na kuitangaza nchi kwa ujumla.
 Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Rachael na Linah wakiwa wamepozi katika picha ya ukumbusho na Mzee Njenje.

TAZAMA PICHA 5::DANSI LA SERENGETI FIESTA LILIVYOCHENGUA JIJI LA TANGA

IMG_2829
Kikundi cha Platinum Dancers kikionyesha umahiri wao wakati wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta, lililofanyika katika Ukumbi wa Klabu Lavida , mjini Tanga ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Serengeti fiesta linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi Agosti 23 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
IMG_2830
Majaji wa shindano la kumsaka mshindi wa  dansi la Serengeti fiesta wakifuatilia kwa makini namna wasanii wanavyotoana jasho ili kumpata mshindi wa shindano hilo.

IMG_2831
Kundi la Street Color, likionyesha umahiri wao katika  kinyang’anyiro hicho ambacho  mshindi aliondoka na kitita cha sh milioni  moja na kupata nafasi ya kutoa shoo katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Friday, August 22, 2014

MAANDALIZI YA FIESTA TANGA JIONEE HAPA

Wataalam wakiendelea na uandaaji wa jukwaa maalum kwa tamasha la Serengeti Fiesta 2014 litalofanyika jumamosi hii pale Mkwakwani JIjini Tanga

Wednesday, June 18, 2014

MISS TANGA 2014 WATEMBELEA MWAMBAO FM


  Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamesimama mbele ya basi lao muda mfupi baada ya kutoka kutembelea kituo cha redio Mwambao Fm jijini Tanga.
  Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamesima mbele ya hoteli ya Tanga Beach Resort ambako wameweka kambi yao kwa wiki ya pili sasa wakijiandaa na shindano hilo litakalofanyika jumamosi hii 21/06/2014 Mkonge Hotel.
Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamelizunguka gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo.
=======  =======  =======
Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 jana walitembelea kituo cha matangazo cha redio Mwambao Fm cha jijini Tanga kujionea jinsi kituo hicho kinavyorusha matangazo yake.

Wakiwa katika kituo hicho, warembeo hao walipata fursa ya kuzungumzia shindano hilo huku kila mmoja akitamba kuibuka mshindi siku ya jumamosi ya tarehe 21/06/2014 ndani ya Mkonge Hotel kuanzia saa moja usiku.

Baadaye leo washiriki hao watatembelea kituo cha redio cha Breeze Fm pia cha jijini Tanga na kesho wanataraji kwenda kutoa msaada katika moja ya vituo vya kulea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Shindano hili limedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Redd's, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm. Malkia wa mipasho Afrika Mashariki, Bi Hadija Omary Kopa ndiye atakayetoa burudani siku hiyo