Monday, August 25, 2014
Saturday, August 23, 2014
WASANII WATAKAOTUMBUIZA TAMASHA LA FIESTA 2014 JIONI YA LEO JIJINI TANGA WAMJULIA HALI MZEE NJENJE NYUMBANI KWAKE SAHARE
Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,almaarufu kama Mzee Njenje akizungumza machache mbele ya wasanii mbalimbali wa bongofleva waliofika nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga,kumjulia hali kutokana na maradhi yake yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa.
Mzee Njenje amewaasa wasanii hao ambao amekiri wazi kuwa wanafanya vizuri katika anga ya muziki wao,kupata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo na suala la kutoendekeza masualaua ya anasa kama vile ulevi,ngono na mengineyo ambayo huchangia kuporomoka kwa wasanii wengi,amesema kuwa Muziki wa sasa una ushindani mkubwa hivyo kila msanii anapaswa kujituma kwa namna anayoona inafaa ili kutimiza malengo yake sambamba na kuitangaza nchi kwa ujumla.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Rachael na Linah wakiwa wamepozi katika picha ya ukumbusho na Mzee Njenje.
TAZAMA PICHA 5::DANSI LA SERENGETI FIESTA LILIVYOCHENGUA JIJI LA TANGA
Kikundi cha Platinum Dancers kikionyesha umahiri wao wakati wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta, lililofanyika katika Ukumbi wa Klabu Lavida , mjini Tanga ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Serengeti fiesta linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi Agosti 23 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
Majaji wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta wakifuatilia kwa makini namna wasanii wanavyotoana jasho ili kumpata mshindi wa shindano hilo.
Kundi la Street Color, likionyesha umahiri wao katika kinyang’anyiro hicho ambacho mshindi aliondoka na kitita cha sh milioni moja na kupata nafasi ya kutoa shoo katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Friday, August 22, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)